MECHI YA TWIGA STARS NA RWANDA YAAHIRISHWA

0
210
Twiga Stars: Wawakilishi wa Tanzania kwenye soka la wanawake

Mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Rwanda uliokuwa ufanyike Jumapili Julai 17, 2016 umeharishwa.

Mchezo huo ulikuwa maalumu kwa burudani kwa wakuu mbalimbali wa nchi za Afrika wanaotarajiwa kuwa na mkutano wa viongozi kuanzia Julai 14, 2016 nchini Rwanda.

Shirikisho la soka nchini Rwanda ‘FERWAFA’ kupitia Rais wake, Nzamwita Vincent limeandika barua kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuahirisha mchezo huo kutokana na kuingiliana na muda wa ratiba ya kwanza kwa mikutano ya wakuu nchi za Afrika.

Twiga Stars: Wawakilishi wa Tanzania kwenye soka la wanawake
Twiga Stars: Wawakilishi wa Tanzania kwenye soka la wanawake

LEAVE A REPLY