Mechi ya Manchester United na Crystal Palace yaacha rekodi

0
169

Mechi ya Manchester United dhidi ya Crystal Palace ambapo iliisha kwa Manchster United kushinda 3-2 imeacha rekodi nchini Uingereza.

Moja ya rekodi ni klabu ya Manchester United kutokea nyuma kwa  mabao 2-0, na kushinda mchezo wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu ifanye hivyo Desemba 2013 ugenini dhidi ya Crystal Palace.

Kwa upande wa Crystal Palace jana ndio ilikuwa mechi yao ya kwanza kupoteza baada ya kuwa wanaongoza kwa mabao 2-0 au zaidi. Pia Crystal Palace hawajashinda mechi 20 sasa dhidi ya United ikiwa ni idadi kubwa ya mechi kuliko timu zote walizokutana nazo.

Rekodi nyingine ni bao la kwanza la Nemanje Matic kwa tangu ajiunge na United huku likiwa ni bao la ushindi la dakika ya 90  kwa United.

LEAVE A REPLY