Mchezaji wa kikapu ametoka jicho akiwa uwanjani nchini New Zealand

0
238

Mchezaji wa mpira wa kikapu nchini New Zealand, Akil Mitchell ametoka jicho wakati akiwa uwanjani akicheza mchezo hu.

Mchezaji huyo wa klabu ya New Zealand Breakers, na alikuwa mjini Auckland kucheza mechi ya NBL ya Australia jana usiku kisa hicho kilipotokea.

Mchezaji wa timu pinzani aliingiza kimakosa kidole ndani ya tundu la kishimo cha jicho na ghafla jicho lake likatoka nje.

Mchezaji huyo mzaliwa wa Marekani alianguka sakafuni akiwa ametumia mikono yake kufunika jicho lake la kushoto na akakimbizwa hospitalini.

Mchezaji huyo wa miaka 24 amesema anakumbuka kusikia mashabiki na wachezaji wake wakiingiwa na wasiwasi.

Alidhani hangeweza kuona tena na kwamba uchezaji wake ulikuwa umefikia kikomo.

LEAVE A REPLY