Mbwana Samatta kuivaa Zimbabwe Jumapili

0
205

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayechezea timu ya K.R.C Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta amekubali kujiunga na kambi ya timu ya taifa kwaajili ya maandalizi ya mechi ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe inayotarajiw akufanyika siku ya Jumapili.

Samatta ambaye pia ni nahodha wa kikosi hicho anatarajia kutua nchini siku ya Jumatano ili kuungana na wenzake kwaajili ya kambi ya siku 3 kabla ya kucheza mchezo huo muhimu kwaajili ya kuimarisha viwango vya ubora wa soka vya Afrika na Dunia.

Kwa sasa Tanzania imeshuhudia ikizidi kuporomoka kwenye viwango vya ubora wa soka Afrika na dunia baada ya kushushwa mara mbili mfululizo.

Kikosi kamili kilichoitwa na kocha Charles Boniface kwaajili ya mechi hiyo ni:

Walinda mlango:

Aishi Manula (Azam FC)

Deogratius Munishi ‘Dida’ (Yanga)

Said Kipao (KT Ruvu)

Walinzi:

Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC)

Michael Aidan (JKT Ruvu)

Mwinyi Hajji, Vincent Andrew (Yanga)

Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC)

James Josephat (Prisons)

Viungo:

Himid Mao (Azam FC)

Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Jonas Mkude, Muzamil Yassin, Shizza Kichuya, Jamal Mnyate (Simba SC)

Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting)

Simon Msuva wa Yanga.

Washambuliaji:

Ibrahim Ajib (Simba SC)

John Bocco wa (Azam FC)

Elius Maguli wa (Oman Club)

Thomas Ulimwengu (hana timu)

Omar Mponda (Ndanda FC)

Mbwana Samatta (K.R.C Genk)

LEAVE A REPLY