Mbwana Samatta aumia tena

0
324

Mshambuliaji wa KRC Genk, Mbwana Samatta ameumia tena kwenye mchezo wa jana wakati timu yake ilipoibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Zulte-Waregem kwenye mchezo wa ligi kuu nchini humo.

Samatta aliumia na kutolewa dakika ya 36 huku nafasi yake ikichukuliwa na mshambuliaji Dieumerci N’Dongala ambapo timu hizo zilikuwa sare ya 1-1, matokeo ambayo yalidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Genk ilifanya vizuri na  kupata mabao mawili yaliyofungwa na kiungo Thomas Buffel dakika ya 59 na kiungo Alejandro Pozuelo dakika ya 90, hivyo kufanya Genk iliyokuwa nyumbani kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3-1.

Katika mchezo huo wa jana usiku nahodha huyo wa Taifa Stars alikuwa anacheza mechi yake ya tano tangu apone maumivu ya mishipa midogo ya goti lake la mguu wa kulia iliyochanika Novemba, mwaka jana.

 

LEAVE A REPLY