Mbunge wa zamani wa Somalia mtekelezaji wa mauaji ya ‘kujitoa mhanga’

0
136

Shirika la habari la AFP limeripoti, kundi la Al-Shabab limemtaja mmoja wa watu wawili waliojitoa mhanga jana na kuua watu 13 wakiwemo wanajeshi 7 kwenye kambi ya kijeshi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa ni mbunge wa zamani wa bunge la Somalia.

Salah Badbado aliyekuwa na umri wa miaka 53 ambaye alikuwa mbunge kwa miaka sita kuanzia mwaka 2004 na kisha mwaka 2010 alitangaza, kupitia mkutano na waandishi wa habari kuwa anaacha kazi ya siasa ili kujiunga na kundi hilo.

Kundi la al-shabab lilijinasibu kuwa wapiganaji wake ndio waliotekeleza mauaji hayo yaliyotokea kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Mauaji hayo yalikuwa yakivilenga vikosi vya kimataifa hususani majeshi ya Afrika (AU) na vikosi vya Umoja wa Mataifa (UN) ambavyo vipo nchini Somalia ili kutuliza ghasia.

LEAVE A REPLY