Mbowe aguswa na kifo cha Mama yake mdogo Kikwete

0
324

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ametoa pole kwa familia ya Rais mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete kwa kufiwa na mama yake mdogo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook na Twitter Mbowe ametoa pole hizo sambamba na kuwaombea kwa Mungu awape ujasiri na nguvu katika kipindi hiki cha kuondokewa na Mama yao.

“Natoa pole za dhati kwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Jakaya Kikwete, familia yake kwa kumpoteza mama na bibi katika wakati ambao walikuwa wakihitaji kuendelea kunufaika na matunda ya umri wake hasa hekima, busara na malezi kutoka kwa Bi.Nuru. Wakati tukimuombea kwa mola marehemu Bi. Nuru alale mahali pema kwa amani, tunaomba pia Mwenyezi Mungu awapatie ujasiri na nguvu familia ya Kikwete kuukabili msiba huu, na awafanyie wepesi katika majonzi ya kuondokewa na mama.”

Bi Nuru Kikwete alifariki jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu na mazishi yake yanafanyika leo Bagamoyo Mjini mkoani Pwani.

LEAVE A REPLY