Mbowe afunguka wabunge wa upinzani kuhamia CCM

0
132

Kiongozi  wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema wabunge wanaokimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanafanya hivyo kwa kuwa huko kuna maslahi na kwamba wana haki ya kufanya hivyo kwa sababu upinzani hauwezi kuwazuia.

Kauli ya Mbowe imetolewa ikiwa siku moja tangu kutolewa taarifa katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa CCM kuwa kuna mbunge na madiwani wanane kutoka upinzani ambao wanamwomba Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli, kuhamia CCM.

Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alidai kuwa wao (CCM) wanatumia fedha, lakini upinzani wanatumia nguvu kutetea wananchi.

Hamahama ya wabunge ilianza Oktoba 30, mwaka huu, baada ya Lazaro Nyalandu (45), aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki tangu mwaka 2000, kujiuzulu kwa madai ya kukosekana kwa demokrasia ya kutosha ndani ya CCM.

Mapema wiki hii kwenye Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Rais Magufuli alisema kwa sasa kuna watu wengi wanaorejea CCM kutoka upinzani na wengine wanaojiunga na chama hicho kwa mara ya kwanza na kwamba yupo mbunge ambaye anamuomba sana kuhamia CCM akiwa na madiwani nane.

LEAVE A REPLY