Mbosso awajia juu mashabiki wake kuhusu kusambaa video yake chafu mtandaoni

0
780

Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka label ya WCB, Mbosso amewalaumu mashabiki wake baada ya video yake kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Moromboso amesema hayo baada ya video yake iliyokosa maadili kusambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha akicheza na mwanamke kimahaba.

Siku chache zilizopita video ilisambaa mtandaoni iliyomuonyesha Mbosso akiiwa stejini akitumbuiza kwenye shoo ya Kusi Night iliyofanyika katika ukumbi wa Dar Live huku akimbambia msichana mmoja katika staili za kimahaba.

Video hiyo ilisababisha mashabiki kumjia juu Mbosso huku wakiwarushia lawama WCB na kudai wamembadilisha Msanii huyo na kumfundisha tabia mbaya.

Lakini pia Mbosso amesisitiza kuwa yeye binafsi hakupenda kufanya vile ila kutokana na msukumo wa mashabiki waliokuwa wanampa ukumbini pale akajikuta akifanya vile.

Baada ya kuposti video hiyo mwanamuziki huyo aliitwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa ajili ya kujieleza sababu ya kupakia mtandaoni video hiyo.

LEAVE A REPLY