Mbosso alivyopitia maisha magumu baada ya kuvunjika Yamoto Band

0
113

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mbosso kutoka lebo ya WCB amefunguka na kusema kuwa alipitia maisha magumu baada ya kuvunjika kwa kundi la Yamoto Band.

Mboso amesimulia msoto aliopitia kwenye maisha yake baada ya kuvunjika kwa Yamoto Band ambapo alikuwa pamoja na wasanii wenzake Aslay, Beka Flavour na Enock Bella.

Mbosso amesema, mara baada ya kusambaratika kwa Yamoto, wasanii wenzake walianza kutoa kazi ila kwa upande wake hakuwa na mbele wala nyuma, jambo ambalo lilimfanya aone maisha ya muziki ni magumu.

Pia amesema kuwa “Binafsi mimi kipindi Yamoto Band imevunjika, nilipoteza mwelekeo kabisa, sikuwa najua cha kufanya.

Amemalizia kusema kuwa Kiukweli nilihangaika huku na kule bila mafaniko, ila ninatoa shukrani zangu za dhati kwa meneja wangu, Mkubwa Fella, amenisaidia sana mpaka hapa nlipofikia,”.

LEAVE A REPLY