Mbosso akanusha kuwa na bifu na Aslay

0
141

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mbosso amekanusha kuwa na bifu na mwanamuziki mwenzake, Aslay ambaye alikuwa naye ndani ya kundi la Yamoto Band.

Mbosso ambaye anatamba na wimbo wake wa Sina Nyota, anasema kuwa, yeye hana shida wala kinyongo na Aslay, kwa sababu haelewi ni nini kinaendelea.

“Mimi na wenzangu tuliokuwa wote Yamoto Band, tuko sawa japokuwa mawasiliano yetu ni hafifu na kila mmoja ana uongozi wake.

“Kuhusu mimi kuwa na bifu na Aslay, naweza kusema sijui nini kilitokea kwa upande wake, maana mimi niko sawa. “Nakumbuka nilikuta amenifuta kwenye ukurasa wake wa Instagram (unfollow), nikashtuka sana na kujiuliza ni kwa nini imekuwa hivyo.

“Watu na kurasa za habari mitandaoni, wakaanza kuposti kitu hicho na sikuchukulia siriazi, nikaamua kuachana na hiyo ishu.

“Nikasema labda kuna mtu alimpa simu yake ndiyo akafanya hivyo au ni mtoto alichezea maana mimi ni mzazi, naelewa mambo hayo.

“Lakini kadiri siku zilivyokwenda, nikaona ni ishu ambayo iko siriazi, sikujua nini kinaendelea mpaka sasa na tangu siku hiyo wala sijataka kujitia ninauliza.

“Mimi sina tatizo, watu wanatakiwa wajue sina tatizo na mtu. “Sijui na wala siwezi kukaa na kinyongo ndani, maana mimi ni mwepesi wa kumwambia mtu neno samahani kuliko neno nakupenda.

Mbosso na Aslay wamepita kwenye mikono ya meneja wa wanamuziki Bongo, Said Fella ‘Mkubwa Fella’.

LEAVE A REPLY