Mbosso afunguka sababu ya kuwa na watoto wawili

0
1544

Mwanamuziki wa Bongo Flava, Mbosso amesema watoto wake wawili wenye umri sawa na kila mmoja na mama yake ni matokeo ya ukuaji ila sio kitu alichokuwa amepanga.

Muimbaji huyo amesema hata hivyo kwa sasa ameshaachana na wazazi wenzie na kila mmoja ameolewa kwa muda mrefu ila anawalewa watoto wake.

Amesema kuwa “Sipendi kuwa muongo na sitakuwa na dhambi ya uongo, huwa inatokea katika ukuaji hususani sisi watoto wa kiume, kuna vitu utajizuia navyo lakini hutashindwa tu,.

Aidha amesema kuwa “Kwa hiyo sitaki kuwa muongo, ilitokea ikawa hivyo nimekuwa baba nina watoto wangu wawili, tunaishi vizuri,”.

Muimbaji huyo kutokea WCB alitambulishwa katika label hiyo January 28, 2018 akiwa ni msanii wa sita kusainiwa baada ya Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen na Lala Lava.

LEAVE A REPLY