Mbinu za Ali Kiba na Diamond Platnumz wakati wa kutoa ngoma mpya ‘hizi hapa’

0
935

Ni wazi kuwa kwa sasa nchini Tanznaia mastaa wa bongo Fleva wenye ‘KIKI’ kubwa ni Diamond Platnumz na Ali Kiba.

Pia mastaa hawa wametajwa mara kwa mara kuongoza kwa mapato kwa wasanii mmoja mmoja huku kazi zao zikipata nafasi ya kushindanishwa na kazi nyingi za kimataifa ikiwa ni pamoja na kushinda tuzo nyingi za ndani na nje ya nchi.

Lakini je, unazifahamu mbinu tofauti zinazotumiwa na menejimenti za mastaa hawa kwaajili ya kuuza biashara zao na kutangaza kazi za wasanii wao?

Diamond Platnumz naye ameweka wazi mbinu yake ya kufanya PUBLICITY na ADVERTISEMENT ya ngoma zake baada ya menejimenti ya Kiba kupitia kwa Seven Mosha kueleza namna wanavyofanya wanapoachia ngoma mpya.

1: Comments za mashabiki

Diamond Platnumz HAJAFAFANUA endapo huwa anashughulishwa na comments za fans LAKINI Mosha alisema wazi kuwa menejimenti ya Kiba huwa ina ‘mute’ comments za mashabiki ili kujiondolea ‘presha’ hususani kwa comments ‘mbaya’.

2: Matumizi ya Redio na Televisheni

Ingawa hizi zimekuwa ndio njia kongwe zaidi za kutangaza kazi za wasanii lakini Diamond Platnumz amesema kuwa njia hizo ‘HAPANA, HAZIFIKIRII’. Wakati Platnumz akizikana njia hizo kongwe, Seven Mosha hajaeleza endapo vyombo hivyo ni sehemu ya mkaakati wa kuzipa promo kazi za Kiba.

3: Mashabiki:

Diamond Platnumz amebainisha kuwa analenga kuwafikia mashabiki moja kwa moja na ndio maana anaenda zaidi kwenye online platforms LAKINI hata menejimenti ya Kiba nayo hili inalizingatia INGAWA inaogopa sana maneno ya mashabiki wasio na busara.

Kwanini Diamond Platnumz haziendekezi redio? MUDA WAKE UMEPITA!

Kwanini menejimenti ya Kiba inafunga comments wakati wa kuachia ngoma mpya? Kwasababu fans wasio na hekima wanaweza kukutoa kwenye kuiamini kazi yako kwa maneno yao tu.

LEAVE A REPLY