Mb Dogg aitupia lawana mitandao ya kijamii

0
128

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mb Dogg amefunguka na kuitupia lawama mitandao ya kijamii na kudai ndio imesababisha wasanii kuharibikiwa kutokana na mitandao hiyo tofauti na zamani.

Kauli ya mwanamuziki huyo inakuja baada ya siku za hivi karibuni kusambaa video chafu za wasanii katika mitandao ya kijamii jambo ambalo MB Dogg amesema siyo zuri kwa jamii.

MB Dogg amefunguka hayo alpokuwa anaongelea baadhi ya matukio ambayo yamewakumba wasanii kadhaa kama Wema Sepetu ambaye anadaiwa kusambaza video zao chafu kwenye mitandao ya kijamii.

Mb Dogg alisema anashukuru viongozi wamekuwa macho na kuchukua hatua lakini anachukia mitandao kwani imefanya watu wengi kuiga kwa kila wanachokiona.

Wema Sepetu wameshachuliwa hatua za kisheria kwani amekishwa mahakamani na kesi yake tayari ishaanza kusomwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

LEAVE A REPLY