Mauaji ya watu 9 yamefanywa na mtu mmoja – Polisi Ujerumani

0
153

Polisi wa Ujerumani wametoa taarifa ya awali ya shambulizi la kutumia bunduki kwenye duka kubwa la kisasa mjini Munich na kusema limetekelezwa na mtu mmoja na hakuna ushahidi wa kuonyesha zaidi ya mtu mmoja kuhusika kwenye shambulio hilo.

Mshukiwa huyo aliyekuwa na umri wa miaka 18 aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakifanya manunuzi kwenye maduka hayo na kuua watu 8 na kisha kukimbia na kwenda kujiua.

Mkuu wa Polisi wa mji wa Munich, Hubertus Andrae amedai kuwa watu 16 wamejeruhiwa wakiwemo watoto wadogo huku watu watatu wakiwa katika hali mbaya.

Taarifa ya polisi imedai kuwa muuaji huyo alikuwa na uraia wa nchi mbili, Ujerumani na Irani na alikuwa mkazi wa mji wa Munich kwa miaka miwili lakini hakuwa na rekodi zozote za uhalifu wala hakuna ushahidi wa kuonyesha uhusiano na makundi ya kigaidi ingawa uchunguzi bado unaendelea.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo msako mkali wa kuwatafuta watu watatu waliodhaniwa kuhusika na tukio hilo ulianza ambapo inadaiwa watu wawili waliondoka kwa kasi na gari baada ya mauaji hayo kutokea lakini polisi wamethibitisha kuwa watu hao wawili hawahusiki na mauaji hayo.

Mwili wa muuaji huyo, ulikutwa umbali wa kilomita moja kutoka eneo la tukio.

Wakati huo huo, Polisi wa Ujerumani wamewaomba watu wenye video za tukio hilo kuziweka mtandaoni ili ziweze kusaidia kwenye uchunguzi.

LEAVE A REPLY