Mauaji: Congo yaanza kusikiliza mshtaka ya wanajeshi wanaoua raia

0
214

Mahakama ya kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeanza kusikiliza kesi zinazowakabili wanajeshi 215 wanaotuhumiwa kuwaua raia ndani na kwenye maeneo ya mji wa Beni uliopo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Miongoni mwa watuhumiwa hao, 80 kati yao ambao ni sehemu ya jeshi la Allied Democratic Forces (ADF) kutoka Uganda, Congo, Rwanda, Kenya, Tanzania na Sudan, walikuwepo mahakamani siku ya Jumamosi kwenye mji wa Beni, kwenye jimbo la Kivi Kaskazini ambapo mashtaka dhidi yao yalitajwa.Mwendesha mashtaka Kumbo Ngoma aliliambia shirika la habari la DPA.

Washukiwa wengine watapelekwa kusikiliza kesi zao wakitokea kwenye magereza yaliyopo nchini humo.

Washukiwa sita miongoni mwa 80 waliofikishwa mahakamani siku ya Jumamosi wanadaiwa kuwaua watu 51 kwa mapanga karibu na mji wa Beni wiki iliyopita.

Makundi ya haki za binadamu wametaja idaidi ya waathirika wa mauaji ya ADF kufikia zaidi ya 1,000 huku waangalizi binafsi wakidai majeshi ya Serikali yanahusika na mauaji hayo.

Watu wanne waliuawa Jumatano iliyopita karibu na mji we Beni wakati wa maandamano ya maelfu ya watu ambao wanaituhumu serikali na walinda usalama wa Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kuwalinda dhidi ya ADF.

 

LEAVE A REPLY