Maua Sama kujenga nyumba

0
300

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama amefunguka na kusema nguvu ya mashabiki katika kumpa sapoti kumemsaidia kuweza kununua gari na sasa kujenga nyumba.

Maua Sama amefunguka hayo baada ya kufanikiwa katika muziki wake ambapo amewashakuru mashabiki wake kuendelea kumsapoti katika kazi yake.

Maua Sama ambaye kwasaasa anamiliki gari aina ya Toyota Rav 4 ambalo alikiri kuwa alinunua kutokana na wimbo wake wa Iokote kufanya vyema Lakini sasa amesema ameweza kununua kiwanja kwa ajili ya kujenga nyumba yake.

Maua Sama alisema kuwa kwa sasa ameanza ujenzi wa nyumba maeneo ya Mbweni jijini Dar es Salaam.

Mwanamuziki huyo ambaye mwisho mwa mwaka wa jana aliachia wimbo wake uliokwenda kwa jina la Iokote aliyoshirikisha Hans Stone ambao ulifanya vizuri na kumuingizia kipato cha hali ya juu.

LEAVE A REPLY