Matonya aachia dunia mapito namba mbili

0
145

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Matonya ameachia toleo la pili la wimbo wake, ‘Dunia Mapito’ na kutoa sababu za yeye kufanya hivyo.

Matonya alieleza kuwa ameachia toleo hilo la Pili kwa nia ya kuwambusha tena watu kwa mara nyingine kuwa Duniani sio makazi ya kudumu kwa wanadamu.

Matonya ameendelea kusema kuwa “Mfano hili janga la Corona, ni ukumbusho tosha wa kuwa tuna kila sababu za kumkimbilia mwenyezi Mungu. Tuombe na kusali sana kwakuwa Dunia Mapito tu”.

Mwanamuziki huyo ni moja ya wasanii ambao wanatumia Sanaa yao kuwakumbusha watu kuhusu janga la Corona linaloendelea kuitesa dunia kwasasa.

Matonya alitamba na wimbo wa dunia mapito miaka ya nyuma kwa kuwatacha watu maarufu waliofariki dunia kipindi hiko nyuma.

Wimbo huo ameutoa maalumu kwa ajili ya kuwakumbusha watu kuwa dunia tunapita na siyo makazi ya kudumu hivyo watambue siku yoyote wataiacha dunia.

LEAVE A REPLY