Mastaa ‘Waliouona mwaka’ lakini ‘HAWAKUJAALIWA’ ‘kumaliza mwaka’

0
517

Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa mwaka 2016 huku tukifahamu fika kuwa megi yametokea yenye mchanganyiko wa hisia, furaha, huzuni, majonzi, huruma, hasira n.k ishikistaa.com inapitia kwa haraka vifo vya mastaa wa burudani waliofariki dunia kabla ya siku ya leo ndani ya mwaka 2016.

Msanii mkongwe wa muziki wa dans kutoka bend ya Sikinde, Shaaban Dede aliwahi kutunga wimbo ambao swali lake nail linalotushughulisha leo…..‘Nani kauona mwaka, ataumaliza mwaka?’

Kwa HAKIKA NI MAJALIWA YAKE MUNGU KUUONA MWAKA NA KUUMALIZA MWAKA!!

Kassim Mapili, mkongwe wa muziki wa Dansi aliyetamba sana na bendi mbalimbali Kilwa Jazz ambayo ilitoka na kibao ‘Naomba nipate lau nafasi’ na kisha bendi ya Nyanyembe Jazz Band ambapo alitamba na ngoma ya ‘Rangi ya chungwa’.

Mzee Kassim Mapili alifariki mwezi Februari.

Staa mwingi wa muziki aliyefariki dunia mwaka 2016 ni Michael Mhina maarufu kama Jon Woka ambaye alikuwa anatamba na kundi la WATUKUTU huku ngoma zao za Hodi Mganga, Yalaah. Jon Woka alifariki Februari

Tasnia ya filamu nayo haikuachwa mbali na hukumu ya Mungu kwani wachekeshaji waliokuwa wanachipukia kwa kasi kubwa Mohammed Abdallah a.k.a Kinyambe na Issa Makombe a.k.a ‘Kundambanda’ wote wawili nao walifariki dunia huku Kinyambe akifariki mwezi Mei wakati Kundambanda akifariki mwezi Julai.

Bongo Fleva ilipoteza tena wasanii wengine wawili kwa mpigo, marafiki Ude Ude na Iku ambao kwa pamoja walikutwa na mauti mkoani Tanga waliposhambuliwa na watu wenye hasira kwa tuhuma za ujambazi.

Ndanda Kossovo a.k.a Kichaa nae ameingia kwenye orodha ya wasanii waliouona mwaka 2016 lakini Mungu hakuwajaaliwa kuumaliza mwaka huo kwani mnamo mwezi Aprili nae alifariki dunia kwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo.

joni-woka

kinyambe-na-matumaini

kundambanda

ndanda-kosovo

LEAVE A REPLY