Mastaa wa Bongo watakavyotoana ‘roho’ Kampala

0
431

Mwaka wa 2017 umeanza na ushindani wa kazi za wasanii umeanza upya na umeanza sambamba na utolewaji wa tuzo kwa kazi bora za wasanii hao.

Diamond Platnumz tayari ameshauanza mwaka kwa tuzo aliyoipata nchini Nigeria kwenye tuzo za TOO EXCLUSIVE.

Je, Diamond ataweza kuuendeleza moto huo mbele ya mastaa Alikiba, AY, Diamond, Vanessa Mdee, Navy Kenzo, Yamoto Band, Harmonize na Ommy Dimpoz kwenye tuzo za Hipipo Music Awards 2017 za Uganda.

Diamond anawania vipengele vinne, mastaa AY, Alikiba pamoja na Navy Kenzo vipengele viwili na wengine kipengele kimoja.

Tuzo zitatolewa Februati 4 jijini Kampala.

LEAVE A REPLY