Masogange kuzikwa mkoani Mbeya

0
707

Muigizaji wa Bongo Movie, Steve Nyerere ametoa taarifa rasmi ya chama hicho yenye mapendekezo kwa familia kuhusu taratibu za msiba wa msanii mwenzao, Agnes Gerard Masogange ambaye alifariki dunia jana jioni katika Kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kikao cha wasanii uliofanyika Leaders Club jana usiku, Steve alisema wao kama wasanii wameridhia kila mmoja kutoa mchango wake wa pesa kwa ajili ya kufanikisha shughuli ya msiba na mazishi ya Masogange.

Pia, amesema wameridhia na kupendekeza mwili wa Masogange uagwe katika Viwanja vya Leaders kesho Jumapili, Aprili 22, 2018 na kuzikwa nyumbani kwao mkoani Mbeya ili wasanii, mashabiki na Watanzania wapate fursa ya kumsindikiza katika safari yake ya mwisho.

Aidha, Nyerere alisema mapendekezo hayo watayafikisha kwenye familia ya marehemu huku akiwashukuru wote waliojitoa kuchangia na kuwapa pole wasanii wakiwemo viongozi wa Serikali na Watanzania kwa ujumla.

LEAVE A REPLY