Mashindano ya magari milimani yaanza nchini Rwanda

0
252

Mashindano ya mbio za magari ya Rwanda Mountain Rally yameanza kutimua vumbi dereva kutoka Kenya Manvir Singh akitarajia kushinda na kuwa bingwa wa Afrika.

Dereva kutoka Kenya Manvir Singh anayeendesha gari aina ya Skoda amefanya vyema katika raundi zilizofanyika asubuhi na kuwatisha wapinzani wake.

Mizunguko ya leo ilikuwa kwenye barabara mbovu za upande wa mashariki mwa Rwanda walipozunguka kilomita 74 mara mbili.

Dereva kutoka Zambia Leroy Gomez akiendesha gari aina ya Mitsubishi amejaribu kutoa upinzani mkali licha ya kupata matatizo ya gari yake kupinduka lakini akaweza kuendelea na mashindano.

Dereva mwingine anayefanya vyema ni Bukera Valery, bingwa mtetezi wa mashindano haya kutoka Burundi akiwa katika gari aina ya Subaru Impreza.

Jumla ya magari 16 yameanza mashindano haya yatakayodumu kwa siku tatu.

Dereva huyo kutoka Kenya Manvir Singh akiwa anahitaji alama 25 za shindano hili la Rwanda ili kutangazwa bingwa wa Afrika kabla hata ya shindano la mwisho litakalofanyika Zambia.

LEAVE A REPLY