Mashabiki wamponda Nick Minaj kisa Rosa Parks

0
27

Mwanamuziki wa Hip Hop nchini Marekani, Onika Tanya Maraj-Petty maarufu kama Nicki Minaj, amejikuta akiporomoshewa matusi na mashabiki pamoja na watu mbalimbali kufuatia kuachia wimbo wake mpya anaodaiwa kumkashifu Rosa Parks.

Katika video aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram, Nicki aliimba baadhi ya mistari katika ngoma hiyo inayokwenda kwa jina la Yikes ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa inamkashifu Rosa.

Rosa ambaye anachukuliwa kama shujaa aliyekuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani miaka ya 1950.

“Hivi ni nini kimekutokea Nicki, umekuwa kichaa? Unapata wapi ujasiri wa kumkashifu mwanamke shujaa aliyekupa heshima mtu mweusi leo hii,” hiyo ilikuwa moja ya komenti katika video hiyo yenye sekunde 51.

Rosa Parks ni mwanamke mweusi aliyepata umaarufu mwaka 1955 baada ya kugoma kumpisha mzungu siti kwenye basi huko Montegomery, hali iliyosababisha kukamatwa, baadaye maandamano makubwa ya watu weusi yalifuata kushinikiza aachiwe.

LEAVE A REPLY