Mashabiki wamjia juu Lil Wayne kisa kifo cha Nipsey Hussle

0
303

Mashabiki wa mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, Lil Wayne wamemjia juu rapa huyo baada ya kutokuonesha ushirikiano kufuatia kifo cha rapa mwenzake Nipsey Hussle.

Nipsey Hussle alipewa heshima ya mwisho siku ya jana kwenye ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles.

Mashibiki wa msanii huyo wamemshushia matusi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Hata hivyo ukimya wa Lily Wayne umehusishwa na sababu za kuzaa na Lauren London aliyekuwa mchumba wa Nipsey Hussle.

Mtoto wa Lil Wayne na London, Comeron Carter jana alipata nafasi ya kutoa neno la rambirambi kwa rappa Nipsey.

Hata  hivyo baada ya maneno ya kejeli na mazito ya mashabiki yamemgusa Lil Wayne na kuamua kuandika kwenye ukurasa wake wa twitter ‘’RIP NIP’’.

Ni siku 12 tu zimepita tangu mfalme huyo wa Los Angles kupigwa risasi kwenye duka lake la Marathon Clothes ambapo rapa Lil Wayne aliposti picha moja tu tangu aprili 8 na haikuhusiana na kifo hicho kitendo kilichosababisha mashabki wake kumjia  juu.

 

 

LEAVE A REPLY