Mashabiki wamjia juu Diamond kuhusu wimbo wa The One

0
629

Baada ya Diamond Platnumz kuachia wimbo mpya ‘The One’ mashabiki wake wameanza kumandamana kutokana na wimbo huo kufanana na wimbo wa mwanamuziki wa Namibi King Teedee.

Mashabiki hao wanataka kujua ukweli kuhusiana na wimbo ‘The One’ kufanana na wimbo wa King Teedee ambao Diamond alishirikishwa na muimbaji wa Namibia aitwaye, King Teedee.

The One wa Diamond ambao ameuachia asubuhi ya leo tayari umeingia trending namba 1 huku tayari ukiwa umeangaliwa zaidi ya mara 500000 kwa masaa machache.

Kwa upande wa wimbo wa King Teedee , ‘One I Love’ uliachiwa tarehe 2 February 2019 na tayari umeangaliwa mara 381,196  kupitia mtandao wa Youtube.

Wadau wa mambo wanadai huwenda Diamond amekubalina na muimbaji huyo wa Zambia kutumia sehemu yake ya wimbo huo pamoja na beat kwa kuwa imezalishwa na producer wake Lizer Classic.

Kutokana na malalamiko hayo si Diamond wala msanii King Teedee aliyejibu kuhusiana na hilo licha ya wimbo huo kuendelea kufanya vizuri.

LEAVE A REPLY