Mashabiki wachukizwa na tabia ya Meninah

0
44

Mashabiki wamechukizwa na tabia ya muigizaji wa filamu Bongo, Meninah Attick baada ya kuposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anafanyiwa masaji na mwanaume.

Meninah aliposti video hiyo akifanyiwa masaji na mwanaume asiyejulikana, jambo ambalo liliwakera wafuasi wake waliosema kwamba, anarudia yaleyale ya mwaka jana.

Baadhi ya wafuasi hao walimshambulia kwa kusema kuwa mambo mengine anajitakia mwenyewe.

“Huyu mwanamke sijui huwa hajielewi? Anajirekodi mwenyewe video zake halafu anakuwa wa kwanza kukimbilia Polisi na kuwaletea shida watu wengine,” aliandika mmoja wa wafuasi wake

Mwaka jana Meninah aliitwa na Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kuhusishwa na kosa la kusambaza video chafu kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo lilimuingiza matatani mwigizaji Mwijaku ambaye mpaka sasa ana kesi ya Makosa ya Mtandao.

LEAVE A REPLY