Mashabiki wa Chelsea wakasirishwa Gary Cahill kuwa nahodha

0
155

Klabu ya Chelsea imethibitisha kuwa beki wa kati wa klabu hiyo Gary Cahill ndiye atakaye vaa kitambaa cha unahodha huku kukiwa na maoni tofauti kwa mashabiki kwenye mitandao yakijamii.

Cahill anachukua majukumu hayo baada ya kuondoka kwa aliyekuwa nahodha wa klabu hiyo John Terry.

Cesar Azpilicueta ametajwa kuwa atakuwa nahodha msaidizi kuelekea katika msimu wa 2017/2018.

Mashabiki wengi wametoa maoni yao katika mitandao ya kijamii wakipinga kuteuliwa kwa Cahill kuwa nahodha. Mashabiki wengi  wanaamini aliyestahili kupewa unahodha ni beki wakibrazil David Luiz.

David Luiz alikuwa katika orodha ya wachezaji ambao walitajwa kuwa wangerithi mikoba ya John Terry kwa kupewa unahodha na kitendo cha kutomteua kimepingwa na wengi.

LEAVE A REPLY