Marombosso akanusha kushindana na Aslay

0
499

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maromboso amekunusha kushindana na Aslay kwenye muziki wake baada ya kuachia ngoma mfululizo.

Kaul hiyo ya Aslay imekuja kufuatia baadhi ya watu kuhoji kuwa Marombosso kuachia nyimbo mfululizo anataka kumfunika Aslay ambaye amekuwa na mtindo wa kuachia nyimbo kila kukicha.

Marombosso ambaye ni mwanamuziki mpya wa WCB amesema kuwa hawezi kshindana na Aslay kwani kila mtu anafanya muziki wake na anachoangalia yeye ni kufika mbali na si kushindana na mtu.

Marombosso alitambulishwa mwezi uliopita kama mwanamuziki mpya wa WCB ambapo hadi sasa ameachia ngoma kama tatu mfululizo kama vile ‘Watakubali’ na ‘Nimekuzoea’ nyinginezo ambazo zinaonekana kufanya vizuri.

Awali Marombosso na Aslay walikuwa wanafanya kazi katika kundi moja la Yamoto Band kabla ya kuvunjika na kila mmoja kufanya kazi kivyake.

LEAVE A REPLY