Marombosso adai hawezi kuingilia mahusiano ya Diamond

0
590

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, kutoka katika label ya WCB, Marombosso ameweka wazi kuwa hawezi kuingilia Mahusiano ya Bosi wake Diamond Platnumz.

Diamond ambaye ni Mkurugenzi wa label ya WCB amekuwa kivutio sana Kwenye mitandao ya kijamii hasa linapokuja suala la Mahusiano yake binafsi na Familia yake.

Mbosso ambaye alijiunga Rasmi WCB Miezi michache iliyopita amefunguka na kusema hawezi hata siku moja kuingilia Mahusiano binafsi ya Diamond..

Mapema mwaka huu mpiga picha maarufu wa Diamond anayejulikana kama Kifesi alifukuzwa kazi baada ya kuingilia Mahusiano ya Diamond baada ya kumshauri arudiane na Zari badala ya Hamisa.

LEAVE A REPLY