Maromboso atambulishwa rasmi WCB

0
595

Aliyekuwa muimbaji wa Yamoto Band, Maromboso amesainishwa rasmi kwenye lebo ya muziki ya Wasafi (WCB) chini ya mwanamuziki, Diamond Platnumz.

Utambulisho rasmi wa mwanamuziki huyo kujiunga WCB umefanyika jana katika ukumbi wa Hayyat Hotel jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na wadau mbali mbali wa muziki nchini pamoja na wasanii.

Baadhi ya wasanii wa WCB
Baadhi ya wasanii wa WCB

Katika sherehe hiyo ya kutambulishwa kwake msanii huyo ametambulisha pia wimbo wake unajulikana kama Watakubali ambao ameanza kufanya chini ya lebel hiyo.

Baada ya utambulisho huo, Maromboso amemshukuru Diamond kwa mchango wake toka aungane nao baada ya kuvunjika kwa kundi la Yamoto Band.

Kwa upande wa Diamond Platinumz ambae ndio kiongozi wa wasanii wa Wasafi amesema kuwa kuanzia sasa hivi mashabika wake wakijua kuwa maromboso ni msanii kutoka kwao.

LEAVE A REPLY