Maromboso afunguka baada ya wimbo wake kufikishwa ‘views’ milioni moja

0
940

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maromboso ‘Mboso’ amefunguka na kusema kuwa amefurahishwa na video ya wimbo wake ‘Watakubali’ kufikisha watazamaji milioni moja kwenye mtandao wa Youtube.

Mboso alitambulishwa na lebo WCB wiki iliyopita ambapo kama mwanamuziki mpya pia aliachi wimbo wake mpya ambao umekonga nyoyo za mashabiki wake.

Baada ya kufikisha views hao ndani ya mtandao huo, Mboso amewashukuru mashabiki wake waliotazama kwa wingi video hiyo kupitia Youtube mara baada ya kuachiwa rasmi.

Mboso ambaye alikuwa memba wa kundi la Yamoto Band amesema kuwa hakuwahi kufikiria hata siku moja kama ipo siku atatoa wimbo na kupokelewa vizuri na mashabiki wake ndani na nje ya nchi.

Wimbo huo uliachiwa rasmi Januari 28 mwaka huu ambapo Januari 29 alitambulishwa rasmi kuwa memba mpya wa WCB.

LEAVE A REPLY