Mark Zuckerberg aahidi kurekebisha mtandao wa Facebook

0
107

Mkurungenzi mkuu wa Facebook, Mark Zuckerberg ameahidi kurekebisha Facebook ikiwa kama malengo yake binafsi ya mwaka 2018.

Katika ujumbe aliyoutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook amesema kuwa amefanya makosa mengi katika kutekeleza sheria na kuzuia utumiaji mbaya wa mtandao huo.

Zuckerberg ni maruufu kwa kujiwekea malengo binafsi kila mwaka tangu 2009. Facebook ilizinduliwa mwaka 2004.

Mitandao ya kijamii yamekoselewa sana kwa kuruhusu habari zisizo za kweli kusambazwa muda kabla ya uchaguzi wa Marekani.

Mtandao wa kijamii wa Facebook umekoselewa kwa kuruhusu matangazo yenye uhusiano na nchi ya Russia wakati wa kinyang’anyiro cha ugombea rais Marekani.

Bw Zuckerburg amesema atatia jitihada katika “maswala muhimu” aliyoyataja kama “kuilinda jamii yetu dhidi ya unyanyasaji na chuki, dhidi ya mataifa yanayoingia kati ya maswala ya mataifa mengine, na kuhakikisha kwamba muda unaotumiwa kwenye Facebook unatumiwa vizuri.”

Baadhi ya malengo yake ya miaka iliyopita yalikuwa kuvaa tai kila siku na kuwinda na kuchinja chakula chake mwenyewe.

LEAVE A REPLY