Marioo: Sifanyi show bila milioni 20

0
43

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hafanyi show chini ya tsh milioni 20 kutokana na soko lake la music kukuwa nchini.

Marioo amesema “Mimi sasa hivi sifanyi show chini ya Milioni Ishirini. Nikifanya show yangu itakuwa ni Milioni Ishirini kwenda mbele, na ndio maana vishow vidogovidogo nimepunguza”.

Pamoja na kuweka wazi dau hilo la show za ndani Marioo hajaweka wazi ni kiasi gani ambacho analipwa kwa show za kimataifa japo amesema kuwa ni zaidi ya Milioni 20 kwakuwa kuna uwekezaji mkubwa hufanyika kuufanya muziki ufike kimataifa.

Marioo amezungumza hayo baada ya kutumbuizia kwenye Tamasha la Simba Day ambalo limefanyika siku ya jana kwa Mkapa.

LEAVE A REPLY