Marioo afunguka sababu ya kuposti picha za kitanzi

0
54

Msanii wa Bongo Fleva, Marioo amenyoosha maelezo kuhusu kutaka kujinyonga kisa kutendwa kwenye suala zima la mapenzi kama ambavyo alivyoashiria kwenye picha alizopost kwenye mtandao wa Instagram.

Marioo amejibu hilo baada ya siku ya kupost picha mbili ikionyesha vitanzi vya kujinyonga huku akiyalaumu mapenzi kwenye maneno ambayo ameyaandika.

“Post zangu mbili tatu ndiyo zimeleta utata kidogo hadi watu kuanza kujiuliza, siku ya kwanza nilipost kitu nikiuliza hivi mapenzi ni kitu gani halafu baadaye nikapost vitanzi ambapo ikaleta utata mkubwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii kwamba Marioo anataka kujinyonga lakini sio kweli ile ni picha tu niliyotumia kwenye cover ya wimbo wangu”

Aidha Marioo ameongeza kusema “Picha ile ilimaanisha kuwa namuongelea mtu ambaye amekata tamaa ya mahusiano hadi kufikiria kujinyonga kwa hiyo nikaamua kuweka kitanzi”.

LEAVE A REPLY