Marioo afunguka kusainiwa Konde Gang

0
285

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo amesema ni ngumu kwake kwasasa kusema atasaini Konde Gang au hawezi kusaini ila tayari ameshafanya kazi na Harmonize.

Marioo ameweka wazi kuwa amefanya wimbo na Harmonize hivyo mashabiki wao wakae tayari tu kuipokea wimbo huo.

”Muda wowote tunatambulisha hilo dude na siku hiyo hakuna kusema kuwa tunatambulisha ngoma bali tunatambulisha muziki.

Pia amesema kuwa hawezi au atasaini, lakini sikuwa na mpango wa kusainiwa na Lebal yoyote maana nina mipango yangu mikubwa” – Marioo.

Marioo pia amepata shavu la kufanya ngoma na Legend wa muziki wa mduara Bob Haisa baada ya kukubali uwezo wake wa kuimba.

Bob Haisa ameeleza anavyomkubali Marioo hivyo hata ngoma watakayofanya itakuwa ni mali ya Marioo yeye hataki chochote kwenye wimbo huo.

LEAVE A REPLY