Marioo adaiwa kupora mpenzi wa mtu

0
37

Mtayarishaji wa muziki nchini Kenya, Magix Enga ametangaza vita na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo kwa madai ya kumtaka kimapenzi mpenzi wake.

Magix Enga amedai kuwa ameachana na mpenzi wake kwa sababu ya Marioo ambaye amekuwa akiumtumia mpenzi wake meseji kupitia DM ya mpenzi wake ambaye hakumtaja jina.

Magix ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram “Nimeachana na mpenzi wangu kwa ajili ya Marioo.

Pia ameendelea kuandika Kwa taarifa yako mimi ndio nilikuwa nachat na wewe mara ya mwisho. Amekuwa akimlaghai mpenzi wangu. Ni bora unifuate mwenyewe kabla sijaanza kupost charts zako”.

Licha yamdai hayo kuibuliwa na mtayarishaji huyo kutoka Kenya, Mwanamuziki Marioo bado hakujibu tuhuma hizo ni kama za kweli au ni uzushi.

LEAVE A REPLY