Maria Careh ‘amehujumiwa’ mkesha wa mwaka mpya?

0
138

Staa mkongwe wa RnB wa Marekani, Mariah Carey ameingia kwenye mzozo na kampuni ya Dick Clark Productions baada ya kuwatuhumu ‘kumhujumu’ onyesho lake la siku ya mkesha wa mwaka mpya.

Mariah Carey alishindwa kuendelea kuimba akiwa jukwaani kwenye ukumbi wa Times Square baada ya viskizi vya masikioni (earpiece) kushindwa kufanya kazi.

Sambamba na hilo timu ya Mariah Carey pia imedai vifaa kadhaa muhimu vilikuwa havifanyi kazi stejini ikiwemo prompter ambayo ilikuwa na mashairi ya kumsaidia kumuongoza Carey.

Hata hivyo kampuni ya Dick Clark Production imeyapinga vikali madai hayo na kusema Carey ndiye aliyekataa kujaribu visikizi vyake kabla ya kupanda stejini.

Pia wamedai kuwa hata kama visikizi vilikuwa havifanyi kazi lakini kulikuwa na spika 8 ambazo angezitumia kusikilizia muziki na kufanya onyesho lake.

Bado haijafahamika endapo Mariah Carey atawafungulia kesi Dick Clark Production au kampuni hiyo itamfungulia kesi staa huyo baada ya kila mmoja kudai amedhalilishwa.

LEAVE A REPLY