Marekani na washirika wake kuimaliza IS?

0
132

Waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter amesema nchi yake na nchi washirika wake kwenye mapambano dhidi ya kundi linalojulikana kwa jina la Islamic State (IS) wamekubaliana juu ya mikakati maalum ya kulimaliza kundi hilo.

Mkakati uliopo ni kuwazingira wapiganaji wa kundi kwenye maeneo mbalimbali ya ngome zao zilizopo nchini Iraq na Syria.

Maeneo hayo ni pamoja na Raqqa (Syria) na Mosul (Iraq).

Hata hivyo waziri Carter ameonya kuwa mkakati huo hauwezi kudhibiti au kumaliza itikadi ya fujo au uwezo wa kuanzisha mashambulizi kwenye maeneo mengine.

Pia nchi hizo washirika zimejadiliana kuhusu mipango ya kuimarisha ulinzi kwenye maeneo ambayo kundi la IS limeondolewa.

Licha ya kushindwa katika maeneo mengi ambayo walikuwa wanayashikilia mwanzoni kundi la IS bado lina nguvu na linashikilia maeneo muhimu kwenye nchi za Iraq na Syria.

Wakati huo huo waziri wa ulinzi wa Uingereza Michael Fallon amesema kuwa nchi yake itaongeza askari wake hadi kufikia 500 ili kuwapa mafunzo wanajeshi wa Iraq na wakurdi kwaajili ya mapambano dhidi ya IS.

LEAVE A REPLY