Marapa watano wa Bongo anaowakubali Madee

0
253

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Hamad Ali ‘Madee’ ametaja wasanii watano wa hip hop anaowakubali zaidi huku akimtaja Fid Q ndiyo bora zaidi kutokana na aina ya mistari yake kwenye nyimbo zake.

Madee amesema kuwa licha ya kumkubali zaidi Fid Q lakini anapenda kupata ushauri wake siku zote kuhusu muziki na maisha.

Madee amesema ukimtoa Fid Q wasanii wengine ambao anawakubali na kupenda kazi zao kutoka Bongo ni Mwana FA, Mr Blue, Roma Mkatoliki pamoja na God Zillah.

Mbali na hilo Madee amesema yeye amejiwekea utaratibu wa kubadili aina ya muziki wake kila baada ya miaka mitano, ili kwenda sawa na soko la muziki la wakati huo na kusema ameamua kufanya hivyo sababu muziki wa sasa unahitaji ujanja ujanja ili mambo yaweze kwenda.

LEAVE A REPLY