Maradhi mapya yanayotishia usalama wa wagonja wodini?

0
166

Polisi wa jimbo la Florida nchini Marekani wamewakamata maafisa uuguzi wawili kwa kosa la kushiriki shindano la ‘vita ya selfie’ kwa kupiga picha na wagonjwa waliokuwa chini ya uangalizi wao.

Kayla Renee Dubois ni afisa muuguzi wa Navarre ambaye alikamatwa Alhamisi na kisha mshindani wake Christopher Wimmer wa Crestview alijisalimisha mwenyewe polisi.

Taarifa ya polisi imedai kuwa wauguzi hao walikuwa wakipiga picha na wagonjwa ambao walikuwa usingizini, wamezimia au kwa namna moja au nyingine hawana fahamu wakati wa kupiga nao picha.

Washtakiwa hao walikuwa wakitumiana picha na meseji zinazoonyesha wingi na uzuri wa picha walizopiga na wagonjwa wao huku wakihamasishana kuongeza ushindani na kuwashirikisha wauguzi wengi zaidi.

Washatakiwa hao wanashtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuwapiga picha wagonjwa bila ridhaa zao (huku wengine (wanawake) wakiwa wazi kwenye baadhi ya sehemu ikiwemo kifuani).

Polisi walianza uchunguzi wa kesi hiyo baada ya kupokea malalmiko ya maafisa uuguzi wengine waliokuwa wakitumiwa picha na ujumbe wa maneno wa kuwahamasisha kushiriki mchezo huo.

Wachunguzi wameshawabaini waathirika 41 wa vitendo hivyo ambapo inadhaniwa kuwa watatu kati yao walitoa ruhusa ya kupiga selfie na wauguzi hao huku 19 wakiwa wanawake, 17 wanaume na wote wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 24-86.

Wagonjwa wawili kati ya hao wamefariki dunia.

Baada ya sakata hilo, Dubois amefukuzwa kazi na Wimmer amejiuzuru.

LEAVE A REPLY