Mapigano: Wanajeshi wanne wa Ufaransa wauawa kwenye helikopta Libya

0
393

Wanajeshi watatu wa Ufaransa wameuawa kwenye shambulio la angani karibu na mji wa Benghazi, nchini Libya baada ya helikopta waliyokuwa wamepanda wakiwa kwenye doria kutunguliwa.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo huku akidai kuwa wanajeshi hao waliuawa wakiwa kwenye utekelezaji wa jukumu la hatari la kiusalama.

Serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imetoa taarifa yake na kudai kuwa uwepo wa askari hao wa Ufaransa kwenye nchi hiyo ni uvunjifu wa mamlaka ya taifa hilo na hivyo haijafurahishwa na taarifa ya serikali ya ufaransa. 

Mapema siku ya Jumatano, msemaji wa wizara ya ulinzi ya Ufaransa, Stephane Le Foll alithibitisha kuwepo kwa mara ya kwanza kuwa askari wa kikosi maalum wan chi hiyo wapo nchini Libya.

Siku ya Jumanne maafisa wa Libya walinukuliwa wakisema kuwa kundi la wapiganaji wa kiislam liliitungua helikopta ya Ufaransa.

Nchi ya Libya imesambaratika kwenye makundi tangu kung’olewa madarakani kwa aliyekuwa rais wan chi hiyo hayati, Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2001 na sasa kuna tawala zinazohasimiana na kila moja ikiungwa mkono na makundi tofauti ya kijeshi hali ambayo imesababisha kundi la IS nalo kuweka kambi kwenye nchi hiyo.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Ufaransa alipohojiwa siku ya Jumatano alidai kuwa kikosi maalum cha Ufaransa kilikuwa Libya kuhakikisha Ufaransa inakuwepo kila mahali kwenye mapambano dhidi ya ugaidi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ufaransa kukiri kuwepo kwa vikosi vyake maalum vya kijeshi kwenye nchi ya Libya ambapo awali ilidai ndege zake zilizokuwa zikionekana nchini humo zilikuwa zinabeba watafiti wa kijeshi.

Mauaji: Moja ya Helkopta za Ufaransa ikiwa kwenye uwanja wa mapambano
Vikosi maalum:   Moja ya Helkopta za Ufaransa ikishusha wanajeshi kwenye uwanja wa mapambano

LEAVE A REPLY