Manji ashinda kesi ya madawa ya kulevya, sasa yupo huru

0
228

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemuachia huru mfanyabiashara, Yusuf Manji katika kesi ya madawa iliyokuwa ikimkabili baada ya mahakama kushindwa kuthibitisha madai hayo.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeha amesema mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutoa ushahidi wa kujitosheleza hivyo mahakama hiyo kushindwa kuthibitisha iwapo Manji anatumia madawa ya kulevya.

Mkeha ameeleza kuwa mahakama imejiridhisha kuwa mtuhumiwa alikuwa bado anatumia dawa mbalimbali kwa matibabu yake kulingana na maagizo ya daktari na dawa hizo zina vimelea vya morphine ambayo pia inaweza kukutwa kwenye heroine,  kwa hiyo maabara ya Mkemia Mkuu ingeenda mbele zaidi kujua morphine iliyokutwa kwa mtuhumiwa imetokana na nini?

Manji alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 akituhumiwa kwamba, kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View, Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroine.

Manji ambaye alikuwa mshtakiwa alikuwa na mshahidi 7 wakati upande wa mashtaka ulikuwa na mshahidi watatu.

LEAVE A REPLY