Maneno ya Stamina baada ya wimbo wake kusifiwa na Rais

0
64

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Stamina amemshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kusifia wimbo wake mpya aliomshirikisha mwanamuziki Profesa Jay unaoitwa Baba.

Kupitia akaunti yake Instagram mwanamuziki huyo ameandika yafuatayo ‘“Sijui nilie sijui nicheke yaani sielewi aiseh kwa furaha niliyonayo,sina neno lingine zaidi ya AHSANTE kwa RAISI WANGU MAGUFULI, kikubwa uhai. ahsante MUNGU.”

 Rais Magufuli ameomba kupigiwa wimbo huo unaoitwa Baba alipokuwa anazindua studio za Channel 10 na Magic Fm.

Rais Magufuli ameomba kupigiwa wimbo huo akiwa ndani ya studio hizo leo ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu aliyoipanga kuifanya jijini humo.

LEAVE A REPLY