Maneno ya Meya wa Ubungo kuhusu Myika kuhamia CCM

0
105

Meya wa Ubungo, Boniface Jacob amewataka wanachadema watulie kuhusu Mbunge wa Kibamba John Mnyika kwani yupo kwenye mikono salama na kwamba kiongozi huyo siyo wa kununulika kwa kuahidiwa vyeo.

Meya Boniface amefikia hatua hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa zinazoenea kwa kasi kwamba Mbunge Mnyika amejivua uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo pamoja na nafasi yake ya Ubunge.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Meya Boniface amerusha jiwe gizani kwa kutuma ujumbe kwa mtu anayempigia simu Mnyika kwa kumshawishi ahame chama kwamba aache kwani wao huwa wanamrekodi.

“Mwambieni Baba yenu aache kupiga simu ovyo, tumemrekodi na tutaendelea kumrekodi tumuaibishee……any time atume sms au apige tena aone…” Meya Boniface.

Ameongeza “Mnyika siyo dizaini ya hao unaowapigia simu na kuwahahidi vyeo na madaraka ya kuhongwa…..Tunakuweka loudspeaker tunakusikiliza tu…..ukikata simu tunacheekaa….Eti unamwambia binadamu mwenzako unamtaka kwa gharama yeyote…….ili nini?

Mwisho wa wiki hii kullikuwepo na habari inayosambaa kwa kasi mitandaoni ikisema kwamba Mnyika amejivua nafasi zake zote za uongozi ndani ya chama.

LEAVE A REPLY