Maneno haya ya Ommy Dimpoz kumaliza BIFF yake na Diamond Platnumz?

0
686

Unaweza ukadhani kuwa baada ya mastaa Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz kutupiana madongo makubwa hadi kutia aibu hadharani kunaweza kukaharibu uhusiano wa kikazi baina ya mastaa hao, UMEKOSEA!

Biahara au kazi haina mfumo huo, yenyewe inakubali kile ambacho kinaleta faida kwenye uwekezaji na staa wa POZ KWA POZI, Ommy Dimpoz yuko tayari ‘KULA MATAPISHI YAKE’ ilimradi biashara ichukue nafasi yake na watu watengeneze ‘mkwanja’.

Dimpoz ameweka wazi kuwa endapo kutatokea dili ya kupiga mzigo na staa yeyote wa kambi ya upinzani, yeye yuko tayari hata kama mtu huyo atakuwa hasimu wake Diamond Platnumz.

‘WCB ni kampuni na ni lebo yenye lengo la kukuza wasanii lakini pia kuwasaidia kupata faida ya vipaji vyao na kama mimi nitaingia kwenye orodha ya wasanii ambao tutapelekea kupatikana kwa faida miongoni mwetu, kwanini nikatae? Amehoji Dimpoz. Nitaenda na nitapiga mzigo na hakutakuwa na stori za nani alimwambia nani nini. Hii ni biashara na biashara inajumuisha mambo yote hayo na kila linalotokea tunalibeba na tunasonga’.

Je, Platnumz atajibu nini kuhusiana na kauli hii ya Dimpoz?

LEAVE A REPLY