Manchester United yatandikwa na Borussia Dortmund

0
147

Klabu ya Manchester United imefungwa goli 4-1 dhidi ya Borussia Dortmund kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika nchini China hapo jana.

Magoli ya Dortmund yamefungwa na Gonzalo Castro aliyefunga magoli mawili dk ya 19 na 82 huku mengine yakifungwa na Emerick Aubemayang kwa mkwaju wa penati dk ya 36 na lingine likifungwa na Ousmane Dembele dk ya 54.

Manchester United walipata goli lao la kufutia machozi kupitia mshambuliaji wao mpya Henrik Mkhitryan aliyetoka klabu hiyo ya Dortmund mnamo dk ya 59.

Manchester United ipo ziarani nchini China kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza ambapo jumatatu watacheza dhidi ya Manchester City.

LEAVE A REPLY