Manchester United wako radhi Marouane Fellaini aondoke bure

0
108

Manchester United watamruhusu Marouane Fellaini kuondoka klabu hiyo bila malipo mwishoni mwa msimu huu kuliko kumuuza kiungo huyo wa kati mwezi Januari.

Mkataba wa Fellaini unakamilika tarehe 30 mwezi Juni na United walianza mazugumzo na Mbelgiji huyo kuhusiana na mkataba mpya msimu uliopita, hadi sasa hakujaonekana makubaliano ya aina yoyote hadi sasa.

Kiungo huyo wa miaka 29, aliikataa ofa ya karibuni zaidi kutoka kwaUnited mwezi Septemba.

Fellaini aliyejiunga na United kwa kima cha £27m mwezi Agosti alikuwa miongoni wa wachezaji bora kujiunga na United meneja David Moyes alipochukua hatamu.

Inafahamika kwamba Fellaini aliamua kuachia bonasi ya £4m ili kuhakikisha uhamisho wake unafaulu.

Thamani yake kwa klabu ya United imeshuka na pia hapendwi tena na mashabiki. Alizomwa na mashabiki wa klabu hiyo mwezi Disemba 2016 alipokuwa akipasha misuli yake moto kuingia uwanjani kama nguvu mpya walipokuwa wakikabiliana na Tottenham katika uwanja wa Old Trafford.

Alifunga bao katika nusu fainali ya ligi ya Uropa dhidi ya Celta Vigo na pia kuanza waliposhinda 2-0 dhidi ya Ajax kwenye fainali.

Fellaini hapo awali alihusishwa na kutaka kuihamia Galatasaray msimu wa majira ya joto.

Lakini Meneja wa United Jose Mourinho alisema klabu ya Uturuki ilikuwa na nafasi nzuri sana ya kumsaini yeye mwenyewe kuliko Fellaini.

Fellaini alikosa kushiriki mechi nyengine msimu huu kutoka na jeraha lakini amefunga magoli manne kwenye mechi tisa alizoshiriki.

Inaaminika kwamba Fellaini amekuwa na uhusiano mwema na Mourinho, jambo ambalo huenda likawa muhimu katika kuamua mustakabali wa mchezaji huyo.

 

LEAVE A REPLY