Manchester United leo ‘uso kwa uso’ na Real Madrid

0
212

Real Madrid leo inatarajiwa kukutana na Manchester United kwenye mechi ya kombe la UEFA Super Cup katika uwanja wa Philip II Arena nchini Marcedonia.

Mechi hiyo inakutanisha bingwa wa klabu bingwa Ulaya ‘UEFA’ pamoja na bingwa Europa ligi kwa ajili ya ufunguzi wa mashindano hayo makubwa kwa vilabu barani Ulaya msimu ujao.

Mechi hiyo inatarajia kufuatiliwa na mashabiki wengi duniani kutokana na ubora wa timu hizo mbili barani Ulaya.

Ikumbwe kuwa timu hizo zilikutana katika mechi za kujiandaa na msimu mpya katika ligi zao nchini Marekani ambapo walitoshana nguzu kwa kutoka 1-1 na Manchester United ikashinda kwa penati kwenye mechi hiyo.

LEAVE A REPLY