Manchester derby nchini China ‘IMEFUTWA’

0
116

Mechi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kati ya miamba ya jiji la Manchester nchini Uingereza, Manchester City na Manchester United ‘IMEFUTWA’.

Taarifa ya hivi punde iliyotolewa kwa pamoja na waandaaji wa mechi hiyo pamoja na timu hizo imethibitisha kuwa mechi hiyo imefutwa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Timu hizo ziko ziarani nchini China na zilitarajiwa kupambana leo hii majira ya saa 9:30 kwa saa za Afrika Mashariki.

China imekumbwa na mafuriko mkubwa kwenye siku za karibuni na tayari mama ya maelfu ya watu wamepoteza makazi yao.

LEAVE A REPLY