Manchester City yapigwa faini ya shilingi milioni 70 na FA

0
124

Klabu ya Manchester City imetozwa faini ya paundi elfu 35 (zaidi ya shilingi milioni 70) na chama cha soka cha Uingereza, FA kufuatia kulalama mbele ya mwamuzi wakati alipotoa adhabu ya penalti kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.

Klabu ya Man city imepewa onyo kwa kushindwa kuwazuia wachezaji wake kuwa na nidhamu uwanjani kiasi cha kumzonga mwamuzi kila wakati.

Hii inafuata tukio la dakika ya 50 baada ya mwamuzi Michael Oliver kuizawadia Liverpool mkwaju wa penalti.

James Milner aliandika bao kwa mkwaju huo wa penalti huku Sergio Aguero akisawazisha dakika ya 69.

Katika mchezo huo ulioisha kwa sare ya 1-1, Gael Clichy alimchezea vibaya mshambuliaji Roberto Firmino wa Liverpool na kusababisha penalti hiyo.

LEAVE A REPLY